About Reconciliation Ministry
Kuhusu huduma ya "Reconciliation Ministry"
Mchungaji George Mamuya amepata maono ya kuanzisha huduma hii ya upatanisho tangu mwaka 2007 na ameendelea kutafuta watu wa kufanya nae huduma hii kwa msaada wa Mungu na bado anaendelea kumsihi Mungu amuongezee zaidi watu waaminifu wa kufanya huduma hii wenye moyo wa kujitoa na moyo wa kidiakonia(Diakonia ni hudpuma kwa jirani mhitaji isiyotegemea faida binafsi ikizingatia upendo na huruma)
Huduma hii ya upatanisho ni pana na imegawanyika katika sehemu zifuatazo
1. Upatanisho wa mtu na nafsi yake.
2. Upatanisho wa mtu na Ndugu yake(watu wengine)
3. Upatanisho wa mtu na mazingira yake
4. Upatanisho wa mtu na Mungu wake
katika halo note yamejengwa katika msingi wa neno la Mungu la kinabii kutoka kitabu cha Isaya 41:10-13
Huduma hii inafanywa na Mungu mwenyewe kwa kuwashirikisha watu wake ili kukuelekeza njia ya kufikia kweke aweze kukupa amani ya moyo wako pale ulipo.
Huduma hii inapatikana kwa njia ya mawasiliano ya ana kwa ana na mawasiliano ya simu.
Ukifika unapokea huduma ya ushauri na neno la Mungu na kisha Mungu mwenyewe anakupa faraja ya kweli uweze kusonga mbele
Ukihitaji amani ya nafsi yako, amani na ndugu yako, amani na Mungu wakona mazingira yako yawe rafiki kwako karibu tuzungumze kisha kwa pamoja tuyapeleke kwa Mungu akupatie haki yako kama ahadi zake zilivyo ya kwamba USIOGOPE *kwa nini usiogope*? kwa sababu yeye yupo pamoja nawe na anakwambia USIFADHAIKE, *kwa nini?* kwa sababu yeye ni Mungu wako, akutiaye nguvu, akusaidiaye na kubadilisha mabaya yote yaliyowazwa juu yako kuwa mema. Hakika *usiogope* wala *usifadhaike* kwa sababu utafika wakati utafute yale yaliyokunyima amani usiyaone.
0 comments:
Post a Comment