Utambulisho


Unaweza kusema nilichonacho ni kidogo, ni kweli kabisa unachosema, ila ukichanganya na changu na cha yule tunaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watoto wa Mungu wanauhitaji upendo wa kweli katika maeneo magumu

Mimi Mchungaji Mamuya nilianzia huduma yangu ya kichungaji katika eneo la misioni tangu mwaka 2013, naweza kusema nimeiona misioni, nimeifahamu misioni, nimeona changamoto za misioni, na nazifahamu changamoto za misioni, nimejaribu kidogo kutafuta utatuzi wa changamoto za misioni, siwezi kusema kuwa nimeshapata jibu la hasha Bali nimeanza kutafuta majibu, tukishirikiana tunaweza kupata majibu sahihi ya changamoto hizi.

Mimi, wewe, yeye na yule  Mungu ametubariki ili na sisi tuwe baraka kwa wale ambao baraka hizo hazijawafikia ili waweze kuona upendo wa kweli wa Mungu katika maisha yao.  (Mwanzo 12:1-3) unabarikiwa ili uwe baraka na baraka hizo zifike kwa wengine. Hebu tujiulize maswali haya:-

1. Mungu alishawahi kukubariki?
2. Baraka ulizopewa umezifanyia nini?
3. Je wengine wamebarikiwa kupitia baraka ulizopewa?

Mungu ametubariki basi nakualika tushirikiane kuifanya kazi ya Mungu kwa Taifa Lake.

Ni mimi mtumwa wa Yesu Kristo
Mchg. George Mamuya
Karibu katika blog yangu hii tufanye kazi ya Mungu







0 comments:

Post a Comment