KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI, JIMBO LA KARATU, USHARIKA WA QURUS
MAHUBIRI YA TAREHE 12/06/2016
SIKU YA BWANA YA 3 BAADA YA UTATU. RANGI YA MADHABAHU KIJANI
MADA: NEEMA YA MUNGU IOKOAYO
MASOMO: ZAB 56:1-13, TITO 3:4-8, *LUKA 8:26-39
SHABAHA: Wasikilizaji waweze kuelewa kuwa ili kupata ahadi za Mungu
tunapaswa kumtegemea Mungu.
“Kwa kuwa mwana wa Adamu alikuja
kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” (Lk 19:10)
UTANGULIZI: Leo ikiwa ni siku ya tatu baada ya utatu tunaangalia
mada izungumzayo juu ya Neema ya Mungu ambayo inatuwezesha sisi kuupata wokovu.
ü
Neema maana yake ni mafanikio aliyonayo mtu
kutokana na majaaliwa ya mwenyezi Mungu au kwa juhudi zake mwenyewe.
ü
Hivyo:- tunaweza kusema kuwa leo tunazungumzia
juu ya mafanikio aliyonayo mtu kutoka kwa mwenyezi Mungu ambayo yanaleta wokovu
katika maisha ya mtu.
ü
Katika kutafakari Neema hii ya Mungu iletayo
wokovu tumepewa kisa kutoka katika biblia Luka 8:26 – 39. Kisa hiki ambacho
kimeelezwa hapa pia kimeelezwa katika kitabu cha mathayo 8:28-34 na kitabu cha
Marko 5:1-20 ikizungumza habari ya mtu aliyepagawa na pepo wachafu ambao
wamejitambulisha kwa jina la Legion maana yake ni jeshi kubwa la warumi lenye
nguvu lililokwa na idadi ya wanajeshi 6000.
Katika kisa hiki unajifunza mambo
yafuatayo:-
- SHETANI NI
MHARIBIFU
Mtu huyu ambaye amepagawa nna
pepo tunaambiwa kuwa alikuwa Uchi, aliishi makaburini, na alikuwa akijikatakata
na mawe (Marko 5:3) Shetani anapoingia kwetu hahurumii hata miilil yetu
atatutaabisha na kuwa wahitaji wakati wote.
- ULINZI WA
KIBINADAMU HAUJITOSHELEZI
Mtu huyu alifungwa kwa pingu na
hata kwa minyororo ila aliikata yote na wanadamu wakakata tama nay eye na
kumuacha alivyo. Unaweza kutegemea wanadamu wanaweza kukusaidia ila ni kwa
kitambo kidogo na utabaki katika shida yako.
- BINADAMU WENGI
WANAANGALIA KITU KULIKO UTU
Tunaelezwa kuwa baada ya mtu huyu
kuponywa watu wa mji ule walimfukuza Yesu kwa sababu walipiga hesabu ya hasara
ya nguruwe 2000 waliofia majini waliona
mwenzao amepata hasara kubwa sasa hawakujua nani angefuata wakaogopa sana wakaamua kumwambia
aondoke kwao.
- MUNGU
ANAJISHUGHULISHA NA MAHITAJI YETU
Yesu alivyoona kuwa mtu huyu yupo
uchi, anaishi makaburini mbali na watu na alikuwa akijikata mwili kwa mawe
alijua kuwa anahitaji msaada hivyo aliona nguruwe hawana umuhimu kama mtu wake akayaelekeza mapepo kwa nguruwe na kumponya
yule kijana. Mapepo yalikwepa kwenda kuzimu yakidani kuwa yakiingia kwa nguruwe
yatakuwa salama ila baada ya kuingia nguruwe walikufa wote na mapepo bado
yakaenda kuzimu.
- UKIMKUBALI
MUNGU UTAKUWA SALAMA
Baada ya mtu huyu kuponywa
alitulia chini ya miguu ya Mungu akiwa amevaa nguo na akiwa na akili yake
timamu. Amani ya kweli inapatikana kwa kumkubali Yesu
- MEMA
ANAYOKUTENDEA MUNGU ANATAKA UMTUMIKIE
Mtu aliyeponywa alitaka kandamana
na Yesu ila yesu alimwambia aende kuelezea habari njema za Yesu kwa watu wa
nyumbani kwake kwa kuwa eneo lile liikuwa ni eneoo la wapagani nao waone wema
wake. Baraka tunazopata tunatumwa tukahubiri.
HITIMISHO
Bora kuwa mlinzi wa getini kwa
Mungu kuliko kuwa mfalme au malkia nje ya Mungu sababu huko hakuna mafanikio ya
kweli, mafanikio ya kweli yaletayo wokovu yanapatikana kwa Mungu tu.
AMEN
0 comments:
Post a Comment