SIKU YA BWANA YA NNE BAADA YA UTATU
19/06/2016
WAZO: SIKU KUU YA KKKT – TUDUMISHE UMOJA WA KANISA
MASOMO” ZAB. 27:1-5, YN 17:22-23, *EFESO 4:1-4
SHABAHA: Kuwafundisha
waumini jinsi umoja ulivyo na nguvu katika kufanikisha kazi ya Mungu.
UTANGULIZI: Umoja
ni nguvu utengano ni dhaifu, walisema waswahili. Hata kanisa letu mwanzoni
lilikuwa na makanisa saba, wakaungana chini ya mwasisis Askofu Stefano Moshi
aliyewaunganisha.
Katika umoja huo kanisa
liliongezeka na hatimaye mpaka sasa zipo dayosisi 24 na maeneo ya misioni 3
haya yote ni matunda ya umoja, pia ni agizo la Yesu, WOTE KUWANA UMOJA Yoh
17:21-23
Katika somo kuna mafundisho tutakayojifunza kuhusu umoja
- KUENENDA KATIKA WITO TULIO ITIWA
Paulo alianza kwa kuwaomba waumini waishi maisha
yaliyostahili wito wao kama wafuasi wa Yesu
Kristo. Anajiita mfungwa kwa sababu maisha yake yametawaliwa na Bwana.
Hata sisi ambao ni wafungwa wa
Bwana maisha yetu yatawaliwe na Yesu kwani tukitawaliwa na Yesu tutashinda
magumu yote kwa upendo alionao Mungu juu yetu.
- WAKRISTO KUISHI KAMA WATOTO WA FAMILIA
MOJA YA MUNGU
Watu wa Mungu wanapaswa kushirikiana kuenenda katika wito
wao walioitiwa, kuwa na maisha ya umoja na kuwa watakatifu, watu waliotofautia
na watu wa dunia hii kuishi maisha safi .
Hata mataifa waasiomjua Mungu wana umoja, lakini umoja unaozungumziwa hapa ni
juu ya watu waliomfahamu Mungu wanapaswa kujenga umoja wao juu ya Mungu.
- UNYENYEKEVU NI TABIA YA MKRISTO
Yesu yeye ni mfano wa kuigwa kwani alitumika badala ya
kutumikiwa. Unyenyekevu ni kinyume cha kiburi, ukiwa na kiburi unaharibu
uhusiano wako na Mungu. Bali unyenyekevu ni
sifa pia ni tabia impasayo mkristo. Hata sisi tunapaswa kuwa na unyenyekevu ili
tuweze kutumika.
- UPOLE UNAJENGA UMOJA
Yesu yeye ni mpole na ni mfano wa kuigwa. Mt 11:28, katika
upoole unaweza kuwasaidia watu kuishi pamoja vizuri, katika upole unaweza
kujitawala kwani utakuwa umetawaliwa na Yesu na anaongoza maisha yako.
- KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU UVUMILIVU
UNAHITAJIKA
Mtu mvumilivu hawi rahisi kukasirika, yu tayari kuvumilia
hata mabaya, yu tayari kusubiri, hafanyi haraka kutafuta haki yake. Hata sisi
uvumilivu ukiwepo hata magumun yakitupata hatuko tayari kukata tama kwa ni
tutavumili kwa Mungu na yeye atatupatia haki yetu.
- HATA KTK UDHAIFU TUNAPASWA
KUCHUKULIANA KTK UPENDO
Kuchukuliana kunajenga upendo kati yetu, iwapo kuna makosa.
Bila kuchukuliana hatuwezi kuonyesha upendo wa Mungu. Upendo unaunganisha
waumini kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Mfano wa mwili unatajwa mwili una
ushirikiano kila kiungo kikiumia mwili wote unaumia. Hivyo hata waumini pasipo
ushirikiano hatutajenga mwili wa Kristo. Mwili wa kristo unajengwa katika umoja.
HITIMISHO
Kwa umoja kanisa la mwanzo liliendelea na kukua sana , hata sisi ambao
tumeitwa na Mungu tutumie vema wito wetu
tulioitiwa kwa kfanya kazi ya Kristo katika kumtumikia Mungu tujivike moyo wa
unyenyekevu, upole, uvumilivu, kuchukuliana, na mambo yanayofanana na hayo.
Katika mambo hayo hakuna hukumu bali tunaweza kuurithi uzima wa milele. Na
uzima wa milele unajengwa katika umoja unaoongozwa na Yesu. Wote tukishirikiana
tutazamie kurudi kwa Yesu kristo na wote tutarajie uzima wa milele. (watumi
5:2) AMEN.
0 comments:
Post a Comment