Wednesday, 31 August 2016

DON'T LET ANYONE LOOK DOWN ON YOU BECAUSE YOU ARE YOUNG

DON'T LET ANYONE LOOK DOWN ON YOU BECAUSE YOU ARE YOUNG(Usikubali mtu yeyote akudharau sababu wewe ni kijana)

Command and teach these things. Don't let anyone look down on you because you are young, but set an example for the believers in speach, in conduct, in love, in faith and in purity. (1 Timothy 4 :11-12).
Wape maagizo haya na mafundisho haya. Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini, ktk usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi. (1Timotheo 4 :11-12)
Siku ya kilele vijana wote walioshiriki walitunukiwa vyeti vya ushiriki, viongozi walipewa pia vyeti vya pongezi na wale waliofanya vizuri kwenye nidhamu, uchapa kazi, na Usafi binafsi nao walipewa vyeti vya pongezi.
Wazo kuu lilikuwa MTU ASIUDHARAU UJANA WAKO likiwa lieberman na kitabu cha 1 Timotheo 4 :11-12
Paulo anamuelekeza kijana Timotheo jinsi ya kuishi maisha safi ya kielelezo na jinsi ya kuliongoza kanisa la Mungu kama kiongozi kijana.
Ni kawaida kwa vijana kutafuta mtu anayeweza kumuangalia ili aweze kupata mfano kwake.
Mungu amekuita wewe uwe mkristo kielelezo kwa ajili yao. Paulo yeye ametaja maeneo muhimu ya wewe kuwa kielelezo :-

KWANZA: Katika maneno yako(usemi) hii ikimaanisha ama ktk maongezi yako uwe makini sana na lugha unayotumia iwe lugha nzuri, au uwe makini katika uelewa wako kwa neno la Mungu. Ufundishe kwa usahihi na uweze kuishi sawa na neno la Mungu linavyoelekeza. Unaposoma ujihoji, neno la Mungu linasema nini? Lini maana gani?  Lina maana gani kwangu, linaniambia nini kuhusu Mungu?  Nk
PILI: Katika mwenendo wako uwe kielelezo kwa sifa ambazo zimeelekezwa katika Waefeso 4:22-30
TATU: Katika kupenda uwe kielelezo, na upendo wenyewe ni wa Agape, upendo ambao wakati wote haupungukiwi na neno lolote kama ulivyofafanuliwa katika 1Korintho 13:1-8
NNE: Katika maisha ya kiroho uwe kielelezo hasa wakati wa majaribu uwe na tabia kama ya Yesu ya upole na unyenyekevu. Kwa sababu watu wengi wapo makini sana kukuangalia ni jinsi gani utakabiliana na majaribu yanayokupata (1Petro 2:21-23)
TANO: Katika imani uwe kielelezo, ni vigumu kumuelekeza mtu amwamini Mungu katika vipindi vya matatizo kama wewe huwezi kumwamini Mungu kwenye kipindi cha matatizo.
SITA: Katika Usafi wa maisha uwe kielelezo, katika mawazo yako, maneno yako, na matendo yako sababu changamoto za ujana ni nyingi, wengine watatamani kuwa karibu na wewe ili tu kutafuta roho yako kuwa makini ukiwaelekeza ktk neno la Mungu.
MWISHO: MUNGU WA AMANI AWAPE BARAKA TELE KWA KUSOMA WARAKA HUU. AMEN.

If you don't allow things to get started, you do not have to worry on how to get them stopped.
Timu ya vijana wa Usharika wa Qurus - Endashangwet
Vijana wa mtaa wa Endashangwet

Vijana waliodumu katika kambi ya vijana Usharika wa Qurus
03-10/07/2016

0 comments:

Post a Comment