Tuesday, 13 September 2016

SIKU YA MCHUNGAJI NA WATOTO TAREHE 10 /09/2016.

SIKU YA MCHUNGAJI NA WATOTO USHARIKA WA QURUS-ENDASHANGWET TAREHE 10/09/2016 MTAA WA MIDABINI
Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kwa mwaka wa Tatu mfululizo kuwa na siku ya Mchungaji na watoto katika usharika wetu wa Qurus-endashangwet. Ni baraka kubwa kukaa na watoto, tuliabudu pamoja nao, walikuwa na kipindi cha maswali ya biblia, walishiriki michezo kama vile wa kuvuta kamba kweli ilikuwa ni furaha kubwa kwangu na kwa watoto. Nilipata nafasi ya kuwafundisha kwa igizo lililoandaliwa nami wakiwa ni mchungaji na wainjilisti naamini kumbukumbu hii njema itadumu kwenye vichwa vya watoto.

Napenda watumishi wenzangu tupate nafasi ya kukaa na watoto, wazazi tuwaruhusu watoto wetu kujifunza kwa uhuru hasa neno la Mungu.

Triangle
Deuteronomy 6:4-9
4 Hear, O Israel: The Lord our God, the Lordis one. Love the Lord your God with all your heart and with all your soul and with all your strength. These commandments that I give you today are to be on your hearts. Impress them on your children. Talk about them when you sit at home and when you walk along the road, when you lie down and when you get up. Tie them as symbols on your hands and bind them on your foreheads. Write them on the doorframes of your houses and on your gates.

(Kumbukumbu la torati 6:4-9)
Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

Watoto ni kitu cha thamani sana ambacho Mungu anawazawadia watoto wake kadiri apendavyo yeye. Inashangaza sana kuona watu wanavyosahau kuwa watoto wametoka kwa Mungu na wanapaswa walelewe kwa upendo na misingi ya neno la Mungu na badala yake wanawaona kama ni mzigo. Jinsi unavyomlea motto tangia akiwa bado mdogo kabisa ndivyo unavyoyajenga maisha yake ya baadaye.

Kwanza kabisa yakupasa uifahamu thamani ya mtoto ambaye Mungu amekupatia. Umhesabu kama zawadi toka kwa Mungu na sio mzigo hata kama haukupangilia kuwa naye kwa wakati huo maana Mungu alishamfahamu kabla hata hajazaliwa. Katika vitabu vya Yeremia na Zaburi tunaona kuwa Mungu anayafahamu maisha ya kila mtoto kabla hata mimba yake yaijatungwa.

Yeremia 1:5a Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;

Zaburi 139:16 Macho yako yaliniona kabla sijakanilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

Tambua kuwa Mungu amekuheshimu na kukupendelea kwa kukupa watoto/ mtoto ili umlee na kumtunza, kwa hiyo yakupasa umpende na kumlea kwa hekima ya ki Mungu na hata siku moja usimuone kama mzigo au kumsema vibaya kwa watu wengine. Hata kama mtoto wako atakuwa na mapungufu kitabia wewe kama mzazi unayemjua Mungu na unaitambua thamani ya mtoto uliyenaye, usimseme vibaya kwa watu bali umuombee, kumuelekeza kwa upendo na kumuonya kwa busara. Fahamu kuwa mtoto wako anathamani kubwa mbele za Mungu naye ndiye anayemjua vyema. Wewe kama mzazi unawajibika mbele za Mungu kwa jinsi unavyomlea mtoto wako ha hivyo yakupasa kujitoa kwa uaminifu katika kimlea kwa upendo na uvumilivu wote.

Tafuta kulifahamu neno la Mungu na kuitafuta hekima ya kiMungu katika malezi ya mtoto wako kuliko hekima ya mwanadamu. Jifunze Mungu anasema nini kuhusu malezi ya watoto na uyafuate hayo kwa uaminifu hata kama kibinadamu  yanaonekana yamepitwa na wakati. Tumia muda kwenye maombi kumwombea mtoto wako na maisha yake ya kimwili na kiroho ili aweze kuongozwa na Mungu siku zote za maisha yake. Mfundishe mtoto wako tangia akiwa na umri mdogo habari za Mungu na kweli yote ya neno la Mungu.  Katika maisha ya siku hizi ni kawaida kuona baba na mama wote wanafanya kazi nje na nyumbani hali inayopelekea watoto kubaki na mlezi muda mwingi wa mchana. Hali hii usipoiwekea mikakati katika malezi ya mtoto wako kiroho inaweza kuleta madhara makubwa hapo baadaye. Hakikisha muda unaoupata kuwa na  mtoto wako unautumia kumweka karibu nawe na kumfundisha habari za Mungu.

Kuna njia nyingi ambazo mzazi unaweza kuzitumia katika kumfundisha mtoto wako habari za Mungu kwa ufanisi kuanzia katika umri mdogo kabisa. Anza kwa kuomba na mtoto wako wakati wote iwe ni asubuhi, wakati wa kula, usiku na wakati mwingine wowote ambao unafanya maombi. Mfundishe kuwa ni muhimu kuomba kabla ya kula na kulala na pia asubuhi baada ya kuamka. Kwa kufanya hivi mara kwa mara basi taratibu ataaza kuona kuwa maombi ni kitu cha muhimu na kadiri anavyokuwa mkubwa ataendelea na tabia ya maombi. Biblia katika kitabu cha mithali  inasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee. (Mithali 22:6).

Msimulie hadithi za biblia kwa njia ya kufurahisha huku ukiwa unamsomea biblia. Mwanzoni itakuwa ngumu kukuelewa lakini kadiri unavyoendelea na kurudia rudia mara kwa mara itakaa ndani yae na itamjengea hamu ya kusoma biblia ili ajue kwa undani zaidi habari ambazo unamsimulia pale atakapokuwa anajua kusoma. Ukiweza mtafutie biblia ya watoto yenye hadithi fupifupi za biblia kwa picha. Waweza pia kutafuta video za hadithi za biblia kwa watoto na mkawa mnaangalia pamoja naye huku ukimsimulia , pamoja na kupata nafasi ya kumfundisha neno la Mungu pia utapata muda mzuri wa kufurahi na mtoto wako na kuwa karibu naye.

Mfundishe kuonyesha shukrani pale mtu anapompatia kitu au kumtendea jambo jema. Hata kama hajui kuongea mwambie sema asante hii itamfundisha kuwa ukitendewa hambo ni lazima kuonyesha shukrani. Mfundishe kumshukuru Mungu kwa kuamka salama, kupata wazaza wanaomlea vyema, kununuliwa michezo mbali mbali, n.k Moyo wa shukrani utamsaidia kumjua Mungu zaidi na atakuwa anatafuta mema ya kumshukuru Mungu kila siku. Ishi maisha ya upendo, furaha, amani na ukarimu wakati wote ili mtoto aone uhalisia wa Mungu katika maisha yako.

Nenda na mtoto wako kanisani kila jumapili  na uwe unamwambia kwanini unaenda kanisani. Usisahau kumpa sadaka naye awe anatoa na umweleze kwa nini tunatoa sadaka kuwa ni njia ya kumshukuru Mungu kwa vingi alivyotupatia. Kumbuka kila mara kumkumbusha upendo wa Mungu, wema na ukuu wa Mungu.

Malezi ya mtoto ni  huduma inayojitosheleza, ni jukumu ambalo umuhimu wake ni mkubwa sana na pale unapokosea matokeo yake kuyabadilisha huwa ni kazi ngumu sana. Mwamini Mungu katika jambo hili na mtegemee na kumtazamia yeye pekee, kama alivyokupa mtoto atakuwezesha kumlea katika njia impasayo.

FAHAMU SEHEMU YA HAKI ZA MTOTO
1. Watoto Wana haki ya kupewa jina na utaifa na kusajiliwa mara baada ya kuzaliwa.

2. Watoto Wana haki ya kutoa maoni yao kuhusu uamuzi unaofanywa ambao unagusa maisha yao, na ni wajibu wa watu wazima kuzingatia maoni ya watoto pale wanapofanya uamuzi huo.

3. Watoto Wana haki ya kufahamu wazazi wao na kuishi nao katika mazingira ya kuwajali na yenye amani.

4. Wazazi na walezi hawana budi kuwalinda watoto dhidi ya madhara yoyote. Vile vile ni lazima wahakikishe kwamba watoto wanapata chakula, mavazi na mahali salama pa kuishi.

5. Wazazi hawana budi kuhakikisha kwamba watoto wanapata kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali

6. Wazazi hawana budi kuwapeleka watoto shuleni na kuwapa nafasi ya kucheza na kupumzika.

7. Watoto Wana Ruhusa ya kufanya kazi baada ya kutimiza umri wa miaka 14. Ila kazi haipaswi kumzuia mtoto kuhudhuria masomo au kupata Muda wa kujisomea na kupumzika.

8. Hakuna anayeruhusiwa kumdhuru, kumuumiza, au kumnyonya mtoto

9. Adhabu kwa mtoto haipaswi kuwa kali au yenye kumdhalilisha.

10. Ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kumdharau mtoto sababu ni msichana au mvulana au sababu ya dini, umri au asili yake.
watoto wakiwa kaaika maandamano ya kuingia katika ibada ya
siku ya mchungaji na watoto tarehe 10/09/2014

Watt zaidi ya 300 wakifurahia siku ya mchungaji na watoto

Watotowakisema mister ya moyo mbele ya wenzao

Watoto zaidiya 300 wakiwasikiliza wenzao wakiimba 

3 comments:

  1. Mchg Hongera Sana kwa blog na post nzuri zinazoonesha huduma za kila siku Usharikani. Mungu akubariki mno.

    ReplyDelete