KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI
USHARIKA WA QURUS – ENDASHANGWET
MAHUBIRI YA TAREHE 03.04.2016
SIKU YA BWANA YA KWANZA BAADA YA PASAKA IITWAYO QUASIMODOGENITI MAANA
YAKE KAMA WATOTO WALIOZALIWA
KICHWA: YESU AJIFUNUA KWA WANAFUNZI WAKE
MASOMO: ZABURI 116: 1 – 8, MARKO 16: 9 – 12, * 1YOHANA 5:1 - 5
SHABAHA: Wasikilizaji waweze kuelewa kuwa maisha mapya ndani ya ya
Yesu aliyefufuka yawawezeshe kuishi maisha mapya yenye ushuhuda.
“Maana umeniponya nafsi yangu na
mauti, macho yangu na machozi, na miguu yangu na kuanguka” (Zaburi 116:8)
UTANGULIZI: Jumapili ya leo ikiwa ni jumapili ya kwanza mara baada
ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo, leo tunajifunza habari za YESU KUJIFUNUA
KWA WANAFUNZI WAKE. Na katika kutafakari hili tumepewa kuangalia neno la Mungu
kutoka waraka wa kwanza wa Yohana.
è Yesu alipojifunua kwa
wanafunzi wake yapo mambo ambayo yalijitokeza kwa wanafunzi wake kama vile
kupata amani, kuondolewa hofu yao, kupewa wajibu wa nini cha kufanya, kuwa na
imani thabiti juu ya Yesu, kuhakikishiwa kuwa Yesu ameushinda ulimwengu na
mauti na mengine Mengi
è Hivyo Yesu
anapojifunua kwetu lazima mabadiliko yajitokeze, tena mabadiliko yenye
matumaini ya kweli.
è Katika somo la Leo
tunajifunza mambo muhimu yafuatayo
- TUNAPASWA
KUZALIWA MARA YA PILI
Ni muhimu na haki kwa kila mmoja
kupata kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya kubatizwa na kumpokea Yesu Kristo
katika maisha yetu ili tuweze kuushida ulimwengu (Yn 3:5-6)
- TUNAPASWA
KUWEKA IMANI YETU KWA YESU KWELI KWELI
Yohana anasisitiza kuwa msingi wa
imani ya kweli ni kumuamini Yesu Kristo kuwa ni mwana wa Mungu aliyetumwa kutoa
sadaka ya maisha yake ili sisi tuweze kusamehewa dhambi zetu kwa kumwamini yeye
tupate kuokolewa.
- IMANI
KATIKA YESU HUDHIHIRIKA KWA UPENDO
KWA JIRANI
è Tunaona wazi kuwa
imani haiwezi kutengwa na upendo kwa ndugu zetu na majirani zetu na kila
ambacho kimeubwa na Mungu.(Kumwamini Yesu ndio mzizi wa kumpenda jirani)
è Bali
yapo mambo ambayo huzuia watu kuwapenda wengine (1 Yn 2:1;2: 15 – 15)
è Tukimtumaini Mungu
atatuezesha kuwapenda ndugu zetu (Rumi 8:33 – 34)
- UPENDO WETU
KWA MUNGU UNAPELEKEA KUSHIKA AMRI ZAKE
èUpendo wetu kwa Mungu
unaonekana kwa njia ya utii, kutii maneno yake na kuzitii amri zake (Yn 4:20,
14:15)
è Kuzishika amari zake
sio kama ni mzigo kwetu bali tuzishike kwa furaha na kuona kuwa ni hitaji letu
ndani ya maisha yetu ya siku kwa siku (Zaburi 40:8; 119:24,35,92.)
- IMANI
KATIKA YESU KRISTO INATULETEA USHINDI KWA DUNIA
Tunapokubali kweli kuiweka imani
yetu kwa Yesu na kukubali kuzaliwa nae na kumruhusu atuongoze katika maisha
haya basi tunahakikishiwa kuwa tutaweza kuushinda ulimwengu. Kwa Lugha nyingine
hakuna njia yoyote inayoweza kuushinda ulimwengu zaidi ya kumwamini Yesu
Kristo.
- HITIMISHO
Tunamwamini Yesu Kristo ili
tuweze kuzaliwa mara ya pili na kuweza kumpenda Mungu, jirani zetu na kuzishika
amri za Mungu ili tuweze kuushinda ulimwengu na zaidi sana kuurithi uzima wa milele.
AMEN.
Mtumwa wa Yesu Kristo mchungaji G. Mamuya |
0 comments:
Post a Comment